Anamtafuta Nani? (A #haiku in Kiswahili)

Akitafuta,
Mali na mamlaka,
Atanikosa,

Akinikosa,
Mali na mamlaka,
Hazina ladha,

Akitafuta,
Busara na uzima,
Atanipata,

Akinipata,
Heshima na uzima,
Nitamwongeza,

Ajipatia,
Heshima na uwezo,
Watamjua,

Wakimjua
Wivu na maadui,
Hatawakosa,

Akinipatia,
Heshima na sifa pia,
Nitamwinua,

Akiinuka,
Njia anazopita,
Nitahifadi.

 

The above is the result of the amalgamation of a series of ideas, and inspiration, drawn from the EQUIP, Classes hosted by Pastor Ken and Catherine Ogalle of Transformation Center Church.